Arsene Wenger: Hatima ya meneja wa Arsenal kuamuliwa

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema hatima yake katika klabu hiyo itaamuliwa katika mkutano wa bodi ya klabu hiyo baada ya fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.
Mfaransa huyo wa miaka 67 amekuwa na Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Wenger amekuwa akishutumiwa sana na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, na kunao ambao wamekuwa wakiweka mabango kumtaka ajiuzulu.
"Kuna mambo mengi ambayo yatajadiliwa katika mkutano wa bodi. Moja, ni nini kitamtendekea meneja," amesema.
"Bila shaka nitakuwepo. Kwa sasa tunafaa kuangazia yaliyopo sasa na ni kwamba tunacheza Jumapili na tuna fainali ya Kombe la FA."
Klabu hiyo ya London kaskazini itakutana na mabingwa wa ligi Chelsea uwanjani Wembley, tumaini pekee la Arsenal kushinda kikombe msimu huu.
No comments:
Post a Comment