Thursday, May 25, 2017


 Man United watashiriki UEFA

Baada ya kukosekana kwa Man United katika michuano ya UEFA Champions League msimu uliyopita kwa kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliyopita na kukosa nafasi ya kushiriki Champions League.
Usiku wa May 24 2017 Man United licha ya kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu, imefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18 baada ya kuifunga Ajax ya Uholanzi magoli 2-0.
Man United wakefanikiwa kuifunga Ajax magoli 2-0 katika fainali ya michuano ya UEFA Europa League ambapo kwa kawaida mshindi hupata nafasi ya kushiriki Champions League moja kwa moja hata kama hajamaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu England.
Mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba ndio alifanikiwa kuifungia Man United goli la kwanza kabla ya muarmenia wa kwanza kuwahi kichezea Man United Henrikh Mkhitaryan kufunga goli la pili dakika ya 48, kama Man United asingetwaa Ubingwa wa Europa asingepata nafasi ya kushiriki Champions msimu ujao.
Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.

Wednesday, May 24, 2017

Timu za Mpira wa Miguu 10 Tajiri Kuliko Zote Duniani


Timu za Uingereza ndizo zinazoongoza kwa kuwa na jumla ya timu tano (Man United, Mancity, Chelsea, Arsenal na Liverpool)  kwenye orodha ya timu 10 tajiri zaidi duniani na zote zikiwa na dhamani ya dola za kimarekani bilioni 8.112, zikifuatiwa na timu mbili (Real Madrid na FC Barcelona) za Uhispania zenye jumla ya dhamani ya dola za kimarekani bilioni 6.43. Timu ya Ujerumani ya Bayern Munich ndio pekee iliyo kwenye 10 bora ina dhamani ya dola za kimarekani bilioni 2.34 huku timu mbili za Uitaliano (Juventus na AC Milan ) zote zikiwa na dhamani ya dola za kimarekani bilioni 1.612

Timu Tajiri kwa Dhamani ya Timu

JinaThamani TimuMapato ya MwakaNchiJina rasmi ya ligi
1.     Real Madrid$3.26 bilioni$746 milioniSpainLa Liga
2.     Barcelona$3.17 bilioni$657 milioniSpainLa Liga
3.     Manchester United$3.10 bilioni$703 milioniUKBarclays Premier League
4.     Bayern Munich$2.34 bilioni$661 milioniGermanBundesliga
5.     Manchester City$1.37 bilioni$562 milioniUKBarclays Premier League
6.     Chelsea$1.36 bilioni$526 milioniUKBarclays Premier League
7.     Arsenal$1.30 bilioni$486 milioniUKBarclays Premier League
8.     Liverpool$982 milioni$415 milioniUKBarclays Premier League
9.     Juventus$837 milioni$379 milioniItalySerie A

Saturday, May 20, 2017

Arsene Wenger: Hatima ya meneja wa Arsenal kuamuliwa

Arsene WengerHaki miliki ya picha
Image captionArsenal wameshinda Kombe la FA mara mbili tangu kushinda ligi mara ya mwisho 2004
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema hatima yake katika klabu hiyo itaamuliwa katika mkutano wa bodi ya klabu hiyo baada ya fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.
Mfaransa huyo wa miaka 67 amekuwa na Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Wenger amekuwa akishutumiwa sana na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, na kunao ambao wamekuwa wakiweka mabango kumtaka ajiuzulu.
"Kuna mambo mengi ambayo yatajadiliwa katika mkutano wa bodi. Moja, ni nini kitamtendekea meneja," amesema.
"Bila shaka nitakuwepo. Kwa sasa tunafaa kuangazia yaliyopo sasa na ni kwamba tunacheza Jumapili na tuna fainali ya Kombe la FA."
Klabu hiyo ya London kaskazini itakutana na mabingwa wa ligi Chelsea uwanjani Wembley, tumaini pekee la Arsenal kushinda kikombe msimu huu.